Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Chakula Bora kwa Uzazi wa Mwanaume

Kula mlo wenye afya na kufanya mazoezi ya kutosha kunasaidia kuweka mbegu za kiume katika hali nzuri. Kwa hiyo ikiwa mnajaribu kupata ujauzito, sasa ni wakati mzuri wa kufikiria kufanya mabadiliko mazuri ya maisha.

Ni mlo gani wa afya unahitajika kwa baba mtarajiwa?

Chakula cha baba mtarajiwa ni tofauti na lishe ya mama mtarajiwa. Kula chakula cha aina mbalimbali kutoka kwa makundi yote ya chakula kila siku:

Angalau sehemu tano za matunda na mboga tofauti tofauti. Hizi zinaweza kuwa safi, zilizohifadhiwa kwenye makopo au kavu, na matunda au juisi, mboga zinaweza kuwa sehemu moja kati ya mlo wa kila siku.

Nafaka zote, viazi na wanga, vitamini muhimu na madini. Hii ni pamoja na mkate, mchele wa kahawia, pasta.

Weka baadhi ya protini katika kila mlo, kama nyama na samaki, mayai, na maharagwe. Jaribu kula samaki angalau mara mbili kwa wiki, ikiwa ni pamoja na samaki wa mafuta.

Bidhaa za maziwa yenye mafuta kidogo kama vile maziwa yenye mafuta kidogo, maziwa mtindi na jibini. Kumbuka kwamba baadhi ya mtindi unaweza kuwa na sukari, hivyo unaweza kupendelea kiasi kidogo cha sukari.

 

Ni virutubisho gani vinaweza kuboresha uwezo wa kupata ujauzito kwa baba mtarajiwa?

Baadhi ya vitamini na madini mengine yanaweza kushiriki katika kukusaidia kupata mtoto. Hata hivyo bado tunahitaji kujifunza zaidi juu ya jukumu halisi la kila virutubisho. Ikiwa unaweza,jaribu kupata vitamini na madini yote unayohitaji katika mlo wako, badala ya kutumia virutubisho(vinavyouzwa –suppliments).

Zinki

Madini ya zinki yana jukumu kubwa katika suala zima la uzazi kwa mwanaume. Uchunguzi juu ya wanaume wenye matatizo ya uzazi unaonyesha kwamba hawapati madini ya zinki ya kutosha ili kuweza kuongeza idadi ya mbegu za kiume na kuboresha kasi yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Vyakula vyenye madini ya zinki ni pamoja na nyama, samaki, vyakula vya maziwa, mkate na bidhaa za nafaka.

Selenium.

Kuna ushahidi kwamba virutubisho vya seliniamu vinaweza kuboresha ubora wa mbegu za kiume, na kutatua matatizo ya uzazi. Selenium ni muhimu katika kuboresha afya ya mbegu za kiume.

Katika utafiti mmoja unaonyesha madini ya seleniamu yanayotumika pamoja na vitamini E yanasaidia kuboresha mwendo wa mbegu za kiume na sura (muundo), na pia kuongeza nafasi ya kupata ujauzito. Kwa hiyo inawezekana kwamba seleniamu ina athari bora kama sehemu ya mlo kamili. Madini ya seliniamu yanatoka kwenye vyakula kama karanga za Brazil, samaki, nyama na mayai.

Vitamini D

Utafiti unaonyesha kwamba vitamini D inaweza kuwa muhimu kwa kusaidia kasi ya mbegu za kiume kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Katika utafiti mmoja mkubwa uliofanyika, ulibaini kuwa wanaume wenye ugumba ndiyo wenye upungufu wa vitamini D ukilinganisha na wale wenye kupata kiasi cha vitamin D kilichoshauriwa.

Miili yetu inahitaji vitamini D kutoka kwenye mwanga wa jua. Vyanzo vizuri vya vitamin D ni pamoja na samaki ya mafuta, nyama nyekundu, ini, viini vya mayai siagi na nafaka zinazoliwa wakati wa kifungua kinywa (cereals).

 Asidi ya foliki.

Labda tayari unajua kwamba ni muhimu kwa mpenzi wako kutumia asidi ya foliki mara tu mnnapoanza kujaribu mtoto. Lakini pia kuna kiasi kidogo cha ushahidi kwamba virutubisho hivi vina jukumu muhimu la kuboresha mbegu za kiume yawe yenye afya.

Antioxidants

Ni aina ya virutubisho vinavyopatikana katika vyakula vya vitamin C au E vinavyosaidia kurekebisha na kulinda seli zilizoathiriwa. Kuna ushahidi unaopendekeza kuwa kupata virutubisho hivi (antioxidants) kwa wingi unaweza kusaidia kulinda ubora wa mbegu za kiume.

Antioxidant vitamin inajumuisha vitamin C na E na Bc, vitamin A pia. Kula matunda na mboga mbalimbali zitakupa antioxidanti nyingi. Weka mfuko wa matofaa (apple) na zabibu kwenye jokofu lako au maeneo ya kazini kwako.

Kuhusu uzito wa baba mtarajiwa

Kuwa na uzito wa afya ni muhimu kwa afya ya mbegu za kiume. Kuwa na uzito mkubwa (BMI zaidi ya 25) inaweza kuwa vigumu kupata ujauzito. Athari hii ni kubwa zaidi ikiwa una (BMI ya 30 au zaidi).

Habari njema ni kwamba kupoteza uzito kunasaidia kuimarisha ubora na wingi wa mbegu za kiume. Pia kupunguza hatari ya magonjwa ya kiafya yanayohusiana na ukosefu wa nguvu za kiume, kama vile ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu.

Kupata uzito wa afya pia itakusaidia kumuangalia mtoto wako mara anapozaliwa kwa urahisi.Kwa hiyo kuna sababu nyingi za kupata uzito wenye afya kabla ya kujaribu kupata mtoto,unapokwama wasiliana na mshauri wako wa afya.

Je,nipunguze matumizi ya kahawa?

Ni vizuri kuendelea kunywa kahawa na chai. Hakuna ushahidi wenye nguvu kwamba kahawa inaweza kuharibu uzazi wako kama baba mtarajiwa.

Kumbuka, baadhi ya vinywaji vyenye kahawa vinatumika kuongeza nguvu vina sukari nyingi. Kama unajiandaa kupata mtoto ni vyema kupunguza matumizi yake.

Vipi kuhusu pombe?

Unywaji mkubwa wa pombe ni mbaya kwa mbegu za kiume inaweza kuwa vigumu kupata mimba. Kwa hiyo, kama ni mnywaji sana unapashwa kuacha ikiwa unataka kuboresha nafasi yako ya kupata mtoto. Inachukua muda wa miezi 3 mbegu mpya kutengenezwa. Hivyo mabadiliko yeyote unayofanya katika maisha yako sasa yatakua na athari nzuri kwenye uzazi wako miezi michache baadaye.