Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mlo Unaoweza Kusaidia Kupata Ujauzito

Mlo wa uzazi unajumuisha vyakula vitakavyosaidia mfumo wako wa uzazi kwa kuimarisha na kusimamia upevushwaji wa mayai na kuboresha nafasi ya kushika mimba na kujifungua salama. Mlo huu unampatia mtoto mwanzo mzuri wa maisha yake.

Tufahamu virutubisho muhimu ambavyo ni muhimu katika kuimarisha mfumo wako wa uzazi:

 • Beta-carotene, phytonutrient, inaimarisha homoni na kuboresha uwezo wa mwanaume vkumpa mwanamke ujauzito.
 • Vitamin B zinazosaidia mfuko wa mayai wakati wa kupevushwa yai na pia kusaidia kuepuka mimba kuharibika. Foliki asidi inasaidia kuepuka matatizo ya neva za fahamu kwa mtoto atakayezaliwa.
 • Vitamin C inasidia kufyonza homoni ya pogesteroni na kumsaidia mwanamke na kasoro za lutea (luteal phase defects).
 •  Vitamin D inasaidia kuboresha uwezo wa kuzaa kwa wanandoa wote. Inachukua jukumu kuu la kutibu matatizo ya uzazi kama uvimbe kwenye mfuko uzazi, uvimbe kwenye mfuko wa mayai, na kuboresha mbegu za kiumekwa mwanaume.
 • Vitamin E inakuza afya ya yai na mbegu za kiume
 • Madini ya chuma yanapunguza nafasi za ugumba unaosababishwa na yai kushindwa kupevushwa.
 • Omega 3 na asidi za fati zinasidia kuboresha idadi ya mbegu za kiume na uwezo wake wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine vilevile na kuongeza kasi ya damu kwenye mfuko wa uzazi.
 • Antioxidants zina kinga na kutibu ugumba.
 • Zinki na selenium zinaimarisha ubora wa mbegu za kiume.
 • Vyakula vyenye fati nyingi vinaweza punguza hatari za ugumba unaosababishwa na yai kushindwa kupevushwa.

Vifuatavyo ni vyakula unavyoweza kuongeza kwenye mlo wako:

1. Mbogamboga za majani

Mbogamboga za majani kama spinachi zina utajiri wa vitamini C na foliki asidi. Pia zinasaidia kuboresha upevushwaji wa yai, utengenezaji wa mbegu za kiumei nzuri na kupunguza nafasi ya mimba kuharibika au magonjwa ya kurithi.

  • Broccoli: zina wingi wa vitamin C ambayo ni muhimu kwenye upevushwaji wa yai
  • Kabichi: ni chakula kizuri kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi. Pia ni chanzo kizuri cha Di-indole methane, ambayo inasaidia kumkinga mama na uvimbe wa mfumo wa uzazi na endometriosis.
  • Viazi: wingi wa vitamin C na kutibu kasoro za lutea kwa mwanamke.
  • Nyanya: Zina wingi wa lycopene, inayosaidia kuboresha idadi ya mbegu za kiume na kuongeza kasi ya mbegu kuogelea.
  • Karoti: chanzo kizuri cha beta-carotene
  • Viazi vikuu: Vina phytoestrogens, ambazo zinahamasisha utoaji wa yai kutoka kwenye mfuko wa mayai na kusaidia kutibu kasoro za lutea kwa wanawake.

2. Matunda

Matunda ni chanzo kizuri cha antioxidants, ambazo ni muhimu katika kuzaa.mfano wa matunda hayo ni:

  • Komamanga: chanzo kizuri cha vitamini C, na inasaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
  • Parachichi:lina wingi wa vitamin B ambayo ni muhimu katika ukuaji wa seli na mfumo wa uzazi, vitamin E,nyuzinyuzi, madini na mafuta muhimu. Vitamin E inasaidia kutunza ukuta wa mfuko wa uzazi.
  • Banana: ina wingi wa vitamin B6 na potasiamu. Inasaidia kuboresha uwezo wa kupata ujauzito kwa kusimamia homoni na kuimarisha ubora wa yai na mbegu za kiume.
  • Zabibu na machungwa yanasaidia kuboresha afya ya yai kwasababu ya wingi wa “polyamine putrescine” ndani yake.
  • Nanasi: kuna imani inayofuatwa inayoaminika kwamba ukila mzizi wa katikati ya nanasi unamsaidia mwanamke kushika mimba kwa siku tano za yai kupevushwa au wakati mbegu imepandikwa ndani ya mwili wa mwanamke kwa njia ya IVF. Nanasi pia lina wingi wa vitamin C inayosaidia kukuza nafasi ya kupata ujauzito kwa mwanaume na kupunguza hatari ya uvimbe kwenye ovari. Nanasi linakuza ubora wa mbegu za kiume kwa wavutaji sigara.

3. Vyakula visivyo mbogamboga

Vyakula hivi ni kama nyama, samaki, na mayai ambavyo vina wingi wa omega3-fati asidi.

  • Mayai: yana wingi wa omega-3, foliki aside na vitamin D.
  • Salmon: ana wingi wa omega 3 fati asidi.
  • Nyama( kuku/nyama): ni chanzo kizuri cha chuma,na fati muhimu.

4. Bidhaa za maziwa

Zina wingi wa kalsiamu, fati nzuri,na vitamin D, bidhaa zitokanazo na maziwa ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa kupata ujauzito kwa wanandoa ambao wanataka kuwa na watoto haraka. Zifuatazo ni baadhi ya bidhaa muhimu za maziwa:

  • Maziwa : yana wingi wa kalsiamu na fati nzuri.
  • Yogurt: chanzo kizuri cha kalsiamu,probiotics, na vitamin D.

5. Miti shamba na viungo

Hii inasaidia kuendeleza usawa wa homoni ya estrojeni kwa mwanake na kusaidia uwezo wa kupata ujauzito.

  • Binzari: Ina wingi wa antioxidants na inasaidia kutibu matatizo yote yanayohusiana na hedhi.
  • Kitunguu saumu: ni kiungo kinachokuza uwezo wa kushika mimba na kina antioxidant inayosaidia mbegu za kiume kusafiri kwa haraka na kuongeza nafasi ya kupata ujauzito ikiwa utatumia siku tano zote za kupevushwa yai.

6. Mafuta na mafuta ya mbegu

Mbali na mbogamboga, matunda, na nyama mbegu na mafuta yake yanachukua jukumu kubwa katika kuboresha nafasi ya kushika mimba. Baadhi ya mafuta hayo ni kama:

  • Mafuta ya Olive: Yanatoa fati zilizo muhimu katika mwili zinazosaidia kupunguza kuvimba mwili kwa ndani na kuongeza umakini wa insulini ndani ya mwili wa mwanamke. Inaboresha nafasi ya kupata ujauzito kwa wanawake waliopandikiza mtoto(IVF)
  • Mbegu za maboga: Zina wingi wa zinki ambayo inasaidia kusimamia afya ya mfumo wa uzazi. Pia zinki inasaidia kuongeza viwango vya homoni ya testosteroni na mbegu za kiume na kuimarisha mtiririko wa damu kwenye ogani za mfumo wa uzazi. Zinki inasaidia kuzalisha mayai yaliyokomaa.
  • Mbegu za alizeti, zina wingi wa zinki.

7. Matunda makavu

  • Almond: wingi wa vitamin E na omega-3 fati asidi
  • Njugu: zina wingi wa omega-3 fati, magnesiamu na nyuzinyuzi zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula. Zinaboresha nguvu za manii na spidi yake pia.

8. Vyakula vingine

  • Kunde na maharagwe: Yana utajiri wa protini, nyuzinyuzi na vitamin B.
  • Nafaka: kama mchele wa kahawia,mtama, ngano nk. Hizi zina wingi wa nyuzinyuzi na husimamia kiwango cha sukari, hivyo kuendeleza kiwango cha foliki aside ili kukuza nafasi ya kupata ujauzito.

Vyakula vya kuepuka ukitaka kupata ujauzito

 • Vyakula vyenye mabaki ya dawa za viwandani za kukuza mazao, kama strawberi, sukumawiki, pilipili, au zabibu, vinapunguza nafasi ya kupata ujauzito.
 • Vyakula vya baharini kama samaki wa maji chumvi, walio na mekyuri nyingi. Mekyuri nyingi inapelekea ugumba na kuharibika mimba.
 • Vyakula vinavyopitishwa kwenye mafuta kama vyakula vya kuoka,vya kukaanga na viwandani.
 • Vyakula vyenye kabohaidreti ulaji wa kabohaidreti ndogo unaweza kuongeza ugumba kwa kuhatarisha viwango vya insulini na “testosterone”. Lakini pia vyakula vyenye sukari na nafaka zilizokobolewa zinaweza kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu na kusababisha ugumba unaosababishwa na yai kushindwa kupevushwa.