Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Jinsi ya Kuandaa Maisha Yako kwa Ujauzito

Nini cha kuwaza kabla ya kuanza kujaribu kutafuta mtoto?

Kabla ya kuamua wewe na mwenza wako jiulizeni maswali yafuatayo:

 • Je, wote mmejitolea kuwa wazazi?
 • Mmewaza vizuri, jinsi gani mtasimamia majukumu ya kumlea mtoto na kuweka usawa kati ya kazi na familia?
 • Mmewaza kwamba kuwa wazazi kutabadilisha maisha yenu na watu wa karibu yenu?
 • Umejiandaa na majukumu ya mtoto kama atakua anahitaji matunzo maalumu?
 • Kama kuna utofauti wa dini baina yenu mmeshajadili ni jinsi gani itamuathiri mtoto?

Kumbuka, kwamba kuwa na mtoto kutabadilisha maisha yenu kwa ujumla.

Je tutaweza kumhudumia mtoto?

Unaweza jisikia kutokua na fedha za kutosha kuanzisha familia, ni muhimu sana mtoto wako apokee matunzo na upendo zaidi ya mahitaji tu, haimanishi sio busara kuweka akiba kabla ya kupata ujauzito

Lini niache kutumia uzazi wa mpango?

Ikiwa unatumia vidonge vya uzazi wa mpango na unataka kupata mimba, acha kutumia mara moja kama uko tayari.

Kujua tarehe yako ya mwisho ya hedhi inaweza kumsaidia mkunga au daktari kukadiria tarehe ya kujifungua mara baada ya kupata ujauzito. Inakupatia pia mda wa kubadilisha maisha yako kabla ya kujifungua. Unaweza kugundua kuwa inaweza kuchukua mpaka miezi sita mzunguko wako kurudia hali yake ya awali.

Ikiwa utapata ujauzito wakati unatumia bado vidonge vya uzazi, acha haraka na muone daktari. Hakuna ushaidi kuwa hatari ya ujauzito kuharibika au kujifungua mtoto mwenye mapungufu inaongezeka mara unapopata ujauzito wakati unatumia vidonge vya uzazi wa mpango. Ila unaweza jiridhisha kwa kumuona daktari.

Kama ulikua unatumia sindano za uzazi wa mpango inaweza chukua mpaka mwaka kurudisha hali yako ya kawaida ya kuweza kuzaa.

Je, nahitaji kubadilisha ninachokula kama najaribu kupata mtoto?

Kula ni jambo la muhimu kama unategemea kutafuta mtoto. Kula mlo kamili mara tatu kwa siku, ukijumuisha mahitaji muhimu na angalau sehemu tano ya matunda na mbogamboga.

Virutubisho vinne muhimu ili kupata ujauzito wenye afya ni pamoja na:

 • Foliki asidi
 • Kalsiamu
 • Chuma
 • Vitamin D

Kuhakikisha unapata virutubisho vyote hivi muhimu, jumuisha yafuatayo kwenye mlo wako:

 • Bidhaa za maziwa
 • Matunda na mboga za majani
 • Nafaka ambazo hazijakobolewa.
 • Protini kutoka kwenye nyama,samaki,mayai na karanga.

Unaweza kutumia vitamin zilizotengenezwa kwaajili ya wanawake wanaojaribu kupata mimba au virutubisho vinavyotolewa kwenye kliniki za wajawazito. Virutubisho hivyo vina gram 400 ya foliki asidi na vitamin B itakayosaidia kujikinga na kasoro kwenye neva za fahamu kama spina bifida kwa watoto wanaokua.

Tafiti zilizofanyika zinashauri matumizi makubwa ya kahawa yanaweza kuathiri uwezo wa kuzaa. Ni vema kuangalia kiasi cha kahawa unachotumia kwa siku.

Je,nianze kufanya mazoezi  kabla sijajaribu kupata ujauzito?

Kufanya mazoezi kabla ya kupata ujauzito inaonyesha mwanzo mzuri wa ujauzito wenye afya. Kujenga bidii,nguvu na wepesi kutakusaidia:

 • Kudumisha maisha yenye uhai kipindi chote cha ujauzito.
 • Kuimarisha hisia zako na kiwango cha nishati ndani ya mwili wako.
 • Kufanikisha uzito unaotakiwa kabla ya kubeba mimba.
 • Kuvumilia mabadiliko ya homoni yanayotokea wakati wa ujauzito.
 • Kuvumilia ukali wa uchungu ukifika wakati.

Kuwa makini na fanya mazoezi kila siku ambayo yananyoosha misuli ya mgongoni itakusaidia kupunguza ukali wa maumivu baadae.

Kama utaweza jenga tabia ya kufanya mazoezi kwenye maisha yako ya kila siku kama kutumia ngazi badala ya lift, kutembea au kuendesha baiskeli badala ya kupanda gari.

Kukimbia ni njia nyingine ya kuweza kuweka mwili wako katika umbile zuri kabla ya kubeba ujauzito. Kama wewe si mkimbiaji mzuri unaweza kuanza kidogokidogo sasa. Ila usianze kukimbia mara unapogundua una ujauzito.