Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Kupevuka kwa Yai (Ovulation)

Ovulation (kupevuka kwa yai) ni pale yai moja au zaidi yanaachiwa kutoka kwenye moja ya ovari (mifuko ya mayai) yako. Hii hutokea karibia na mwisho wa muda ambao  unaweza kupata ujauzito katikati ya mzunguko wako wa hedhi.

Kila mwezi, kati ya mayai 15 hadi 20 yanakua ndani ya mfuko wa mayai yako. Yai lililokomaa zaidi hutolewa na kusukumwa kwenye mirija yako ya uzazi (fallopian tubes) inayounganisha mfuko wa mayai na tumbo lako la uzazi. Mifuko ya mayai haipokezani kutoa yai lililokomaa kila mwezi,hali hii inatokea bila mpangilio maalumu.

Lini naweza kupata ujauzito?

Ili kupata ujauzito kwa njia ya kawaida, moja ya yai na mbegu kutoka kwa mwenza wako lazima vikutane kwenye mirija yako ya uzazi. Yai lako haliwezi kuwa hai kwa zaidi ya saa 24 baada ya kuwa kupevushwa. Kwa hiyo kukutana kwa yai na mbegu lazima kutokee ndani ya muda huu.
Kwa upande mwingine, mbegu za mwanaume huweza kuwa hai hadi kufikia siku saba. Zitaishi kwa raha kwenye uke, mfuko wa mimba, au kwenye mirija ya uzazi kwa muda wote huu.
Kiuhalisia una jumla ya siku sita kwenye mzunguko wako ambazo unaweza ukapata ujauzito. Kwa hiyo ukifanya ngono katika kipindi hiki, yai lako lililopevuka tayari linaweza likakutana na mbegu yenye afya na kuchavushwa(fertilized).

Ni wakati gani kupevuka kwa yai kunatokea?

Kupevuka kwa yai mara nyingi hutokea kati ya siku 12 hadi 14 kabla ya hedhi kuanza. Hii ni wastani tu wa makadirio, hivyo inaweza ikawa ni siku chache kabla au baada ya hedhi.

Kwa mfano, tuseme una mzunguko wa kawaida wa hedhi wa siku 28. Hesabu siku ya kwanza ya kuona hedhi yako kama siku ya kwanza. Siku za wewe kuweza kupata mimba ni kati ya siku ya 10 hadi ya 15.

Vilevile, wanawake wengi wana mizunguko inayotofautiana. Kupevuka kwa yai kunaweza kutokea wiki moja kabla au baada ya kuona hedhi yako, ila kutofautiana mwezi mmoja hadi mwingine.

Dalili za yai kupevushwa ni zipi?

Utaanza kuziona dalili za kuwa kwenye “ovulation”siku tano kabla ya yai kupevuka. Kujaribu kuelewa mzunguko wako kwa kutumia tarehe za mzunguko wako pekee haitakupa majibu sahihi. Ndio maana kuna umuhimu wa kuelewa na kugundua dalili za mwili wako kipindi upo kwenye ovulation ili kufanikiwa kupata ujauzito.
Dalili kuu na viashiria vya yai kupevuka vinajumuisha:

  • Mabadiliko ya uteute uliopo kwenye mlango wa uzazi.
  •  Kuongezeka joto la mwili.
  • Maumivu ya tumbo.
  • Maumivu ya maziwa yanapoguswa.
  • Kuwa na hamu ya kufanya mapenzi kuliko kawaida.

Mabadiliko ya ute kwenye mlango wa uzazi
Ute wa mlango wa uzazi ni uteute unaona kwenye chupi au kwenye “toilet paper” unapokwenda kukojoa. Mabadiliko ya ute wa mlango wa uzazi ni alama ya kuwa upo kwenye siku nzuri za mimba kutungwa. Baada ya hedhi kuisha uteute kwenye via vya uzazi unaongezeka kwa ujazo na hubadilika pia hali yake.

Mabadiliko haya yanaendana na kuongezeka kwa kiwango cha homoni ya “Oestrogen” kwenye mwili wako. Pia inaonesha umekaribia muda wa yai kupevuka.

Utakuwa zaidi kwenye uwezo wa kupata mimba kama uteute ule unakuwa kama hauna rangi (clear), unateleza sana na unavutika. Utafanana kama sehemu nyeupe ya yai ukilivunja. Huu uteute huzisaidia mbegu kuwa na kasi zaidi wakati zinaogelea kuelekea kwenye mfuko wako wa uzazi. Uteute huu unazilinda mbegu zinapokuwa zinasafiri kuelekea kwenye mirija yako ya uzazi (fallopian tubes) kukutana na yai lako.

Maumivu ya tumbo
Mwanamke mmoja kati ya watano huwa anasikia kitu kinaendelea kwenye mifuko yao ya mayai (ovaries) wakati wa kipindi cha kupevushwa yai. Hii inaweza ikatokea kama maumivu madogo madogo au maumivu yanayovuta na kuachia.
Kama ukihisi dalili hizi katika kipindi hiki kila mwezi, angalia uteute wa mlango wako wa uzazi pia. Maumivu ya kipindi cha “ovulation” yanaweza yakawa ni njia ya kukuwezesha kutambua kuwa una uwezo wa kupata ujauzito.

Hisia za mapenzi
Hisia za kimapenzi, kuongea au kujitongozesha sana zinaweza kuwa ni dalili.
hamu ya kufanaya mapenzi inakua juu sana katika kipindi hiki. Utatambua mwenza wako anakuwa karibu zaidi na matokeo yake anakua msikivu zaidi. Hili lina ushahidi wa kidaktari!
Baadhi ya dalili zifuatazo zinaonyesha uko katika kipindi hiki lakini si rahisi kugundua:

  • Kuonekana na kujisikia vizuri: kujihisi una mvuto zaidi kimuonekano kadiri unavyokaribia “ovulation”. Kwa mfano unaweza ukajikuta unachagua nguo zinazokuvutia na kuvutia wengine zaidi kimapenzi kwenye kipindi hiki.
  • Manukato ya mwanamke: unanukia vizuri katika kipindi hiki. Harufu ya mwili wako ni nzuri na inawavutia wanaume kimapenzi katika kipindi hiki. Harufu hizi zinaweza kuwajulisha watu upo katika kipindi cha“ovulation”.

Nitawezaje kuongeza uwezo wangu wa kupata ujauzito?

Jaribu kufanya ngono kila baada ya siku mbili au tatu. Mbegu zinazoogelea vizuri ndani ya mwili wako zitakuwa tayari siku yoyote ukiwa kwenye “ovulation”. Mara kwa mara kwenye mzunguko wako wote inakupa uwezo mkubwa wa kupata ujauzito.

Kufanya ngono wakati via vya uzazi wako vina uteute unaoteleza na upo kwenye hali ya kuzipokea mbegu utaongeza uwezo wako wa kupata ujauzito. Kwa wapenzi wenye uzazi salama, wana uwezo kati ya asilimia 20 hadi 25 ya kupata ujauzito kwa kila mzunguko wa hedhi. Zaidi ya asilimia 80 ya wanawake chini ya miaka 40 ambao hufanya ngono kwa kawaida bila kutumia uzazi wa mpango hupata mimba kila mwaka. Zaidi ya asilimia 90 ya wenza wapya hupata ujauzito ndani ya miaka miwili.

shares