Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Mtoto Mwaka 1 na Miezi 3 – (Miezi 15)

Miezi 15 wiki ya 1

Jinsi mwanao anavyokua.

Mwanao anakuwa haraka sana. Anaweza akawa ameanza kupiga hatua mbili tatu na unaweza ukawa umeona anaanza kula mwenyewe.

Kila mchezo achezao unamfundisha zadi kuhusu dunia, hata kama ni kutambua sehemu za mwili au ni kuangusha na kuokota vitu mbalimbali huku na kule

Uelewa wa mwanao unapozidi, anatambua kuwa na yeye ni mwanadamu, na sio tu sehemu ya wewe bali unaweza kutambua pale akijiona kwenye kioo na kijinyooshea kidole. Akijitambua na kuelewa kuwa ni yeye anajiona.

Kuelewa kuwa yeye ni mtu huru kunaweza kuwa na mabaya yake. Na inawezekana kuwa yeye na wewe mkawa tofauti, hivyo uondokapo inaweza kuwa changamoto bado.

Mpaka sasa unaweza ukawa umetambua tabia ya mwanao na unaweza kutambua atakavyofanya ifikapo hali fulani.

Mwanao anaweza akawa mrahisi au mgumu kubadilika kulingana na hali, jaribu kuweka anachopendelea maanani kama unajua anatakiwa apumzike kipindi fulani ili asichoke sana , usiwe na mipango ya kumfanya akose kupumzika

Miezi 15 wiki ya 2

Jinsi mwanao anavyokua

Katika kipindi hichi, neno hapana linaweza kusemwa sana, kati yako wewe na mwanao.

Tabia ya kurudiarudia inaweza ikawa yakuchosha sana, lakini huonyesha kuwa mwanao anaanza kutambua anachopenda na asichopenda kwahiyo usishangae akikuhangaisha wakati wa kuvaa nepi au kupiga mswaki,nk.

Baadhi ya vitu havitakua vya makubaliano kati yako na mwanao, ni vyema atambue kuwa tabia mbaya haikubaliki.

Miezi 15 wiki ya 3

Jinsi mwanao anavyokua

Funguo, penseli lipustiki vinaweza vikawa vitu vya kumfurahisha sana mwanao, hata hivyo wewe ndio mtu wa muhimu maishanimwake kwahiyo vyote vinavyomfanya awe kama wewe ni jambo la furaha sana kwake

Mambo mengi mwanao anayoyapenda kucheza nayo yanaweza yasiwe mazuri sana, kwani vinaweza kumkaba akiweka mdomoni, kwahiyo tafuta vitu anavyoweza kucheza navyo na vikawa salama kwake

Chukua nafasi hii ya mwanao kutambua vitu na umfundishe vitu vizuri kuchezea, unaweza kutumia vitu mbalimbali ambavyo ni salama kwake kuweza kumfundisha mwanao mambo mbalimbali.

Miezi 15 wiki ya nne.

Jinsi mtoto anavyokua

Mwanao anaweza akawa anaota meno wakati huu, kwahiyo jiandae kwa mabadiliko ya tabia yake wakati huu hasa kwenye kula na kunywa.

Punguza maumivu ya meno ya mtoto kutoka kwa kumsugua fizi zake mara kwa mara kwa vidole safi, au kumpa kitu cha baridi aweze kukilambalamba, kama vipande vya matango yenye baridi kwa mbali, kama haisaidii unaweza kutumia dawa maalumu ya meno ya mtoto.

Katika wakati huu uunavyozidi kusema acha ndivyo atakavyo anza kulizoea na kulipuuza hilo neno. Jaribu kutengeneza mazingira mazuri ya kuepuka kulisema neno hilo kila wakati