Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 12

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya kumi na mbili
Sehemu tofauti za uso wa mtoto wako zinaanza kuonekana kama binadamu zaidi. Matundu mawili yanachukua umbo lake chini ya masikio. Macho yake, ambayo yalianza nje kwenye pande za kichwa chake yamehamia karibu zaidi pamoja.
Sasa ni wakati ambapo tishu na viungo vilivyo tayari katika mwili wa mtoto wako hukua kwa kasi na kukomaa. Matumbo ya mtoto wako, ambayo huanza nje kama uvimbe mkubwa katika kitovu, yataanza kusonga kuingia tumboni (belly cavity) kuanzia sasa.

Dalili ujauzito katika wiki ya kumi na mbili
Kwa bahati kichefuchefu chako hivi karibuni kitaisha na kuanza kujisikia vizuri zaidi.
Unaweza tambua kwamba fizi za meno yako zinatoa damu zaidi kwa sasa. Hii kikawaida pia husababishwa na ujauzito wenyewe. Kwa upande mwingine kutokwa na damu kwenye fizi kipindi cha ujauzito inaweza ikasababisha matatizo mengine makubwa zaidi kama isipotibiwa mapema. Hakikisha unapiga mswaki mara mbili kwa siku, na vile vile kumuona daktari kwa ushauri zaidi.

Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya kumi na mbili
Inawezekana umeshafanya skani ya tarehe (ultrasound) kwa sasa. Kama bado basi itabidi ifanyike ndani ya wiki hii au ijayo mwanzoni. Na ifikapo mwisho wa wiki hii hatari ya kupoteza ujauzito itakuwa imepungua sana. Hatua hizi kufikiwa inamaanisha ni wakati muafaka kuiambia dunia kuwa wewe ni mjamzito.