Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 22

Jinsi mtoto wako anavyokuwa katika ujauzito wiki ya 22
Mtoto wako sasa ana mwonekano kama wa kitoto kichanga kabisa. Japokuwa bado ana safari ndefu ya kukua kabla ya kuweza kuzaliwa. Haja kubwa ya mtoto wako pia imeanza kujikusanya kwenye tumbo lake. Haja hii imetengenezwa na vitu mbalimbali ikiwemo maji ya uzazi na seli ngozi zinazopukutika toka mwilini mwake. Atameza vitu hivi na kuvihifadhi tumboni mwake kama “meconium” yenye rangi nyeusi au kijani nyeusi inayonatanata.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 22
Kung`aa kwa ngozi yako ni ushahidi kwamba homoni za ujauzito zinasumbua pia. Unahifadhi zaidi unyevunyevu chini ya ngozi yako kuliko kawaida na pia damu inayozunguka mwilini kwako imeongezeka. Nywele zako pia zina muonekano mzuri. Shukrani kwa ongezeko la estrogeni mwilini mwako, nywele zako zinakua kwa muda mrefu zaidi kabla hazijaanza kudondoka.

Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya 22
Si lazima usubiri mpaka mtoto wako azaliwe ndio uanze kuwa karibu nae. Kuna njia mbali mbali wewe na mwenza wako mnaweza kujisikia karibu na mtoto wenu kabla hajazaliwa. Kukandakanda “massage” tumbo kwa taratibu ni njia nzuri ya kuwa karibu na ujauzito wako. Siku ya kwanza mtoto wako atacheza baada ya wewe kukandakanda tumbo itakuwa ya furaha sana. Mkando wa tumbo pia unaweza kusaidia mzunguko wa damu na kuboresha