Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 26

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 26
Kama ungeweza kumuona mtoto wako kwa sasa, ungeweza kuwa na uwezo wa kupata mtazamo wa macho yake, ambayo yanaanza kufunguka.

Mtoto wako anazidi kupata uwezo wa kuitikia miito ya sauti zaidi kadri wiki zinavyopita. Mwanzoni, anaweza kusikia sauti za chini kutoka ndani ya mwili wako, kama vile mapigo ya moyo wako na kutetema kwa tumbo lako. Lakini kwa sasa, ana uwezo wa kusikia sauti za juu zikipigwa kutoka nje ya tumbo lako (mji wa mimba).

Dalili za ujauzito katika wiki ya 26
Unakaribia kuifikia miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wako. Miezi mitatu yako ya mwisho huanza wakati umekamilisha wiki 27 za ujauzito. Hivi punde,utakuwa umemshika mtoto mikononi mwako na kuanza kumnyonyesha.

Wakati huu, unaweza kuona kuongezeka kidogo kwa shinikizo la damu yako, ambayo ni ya kawaida. Sharti moja wakunga wako watakuwa macho sasa ni kuhusu shinikizo la damu kipindi cha ujauzito (pre-eclampsia). Shinikizo la damu linahusiana sana na (pre- eclampsia).

Hata hivyo, kwa asilimia ndogo kama pre-eclampsia haitatambulika mapema, dalili zake ni pamoja namaumivu makali ya kichwa, kuona maruerue na mikono na miguu kuvimba. Hivyo ni vyema kumuona daktari mara moja pale unapoziona dalili hizi zinatokea. Soma kuhusu dalili nyingine kipindi cha ujauzito ambazo unapaswa kutokupuuzia.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 26
Kama ulifanya kipimo cha “vaginal swab” kuangalia kama una maambukizi ya uke wakati wa ujauzito kama vile muwasho, candida na bakteria, matokeo yake yanaweza kurudi chanya kwa bakteria wa kundi B streptococcus. Haya ni maambukizi ya kawaida ambayo wanawake wengi wanakuwa nayo bila kujua na bila kusababisha madhara yoyote, isipokuwa katika hali nadra sana. Kama utakuwa unapata homa na kupata maumivu makali wakati wa kukojoa ni vyema kumuona daktari.