Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 30

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 30
Kuanzia sasa, mtoto wako anaongezeka uzito haraka. Mapafu yake na njia ya utumbo karibu zinakomaa na yeye pengine atakuwa na uwezo wa kufungua na kufunga macho yake kwa sasa, ili aweze kuona ndani kwako. Kama ukiangazia mwanga juu ya tumbo yako, mtoto wako anaweza hata kujinyoosha ili kujaribu kuugusa mwanga unaosogea.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 30
Pengine umeongezeka uzito kiasi mwezi huu. Kuongezeka gramu 450 kwa wiki ni kawaida kabisa wakati wa miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito. Mahitaji ya mtoto wako ya virutubisho ni makubwa kwa ukuaji wake wa mwisho kabla yeye kuzaliwa.

Unaweza kuwa na furaha kikamilifu na kuongezeka kwaukubwa wa umbo lako.Kama uzito unaoongezeka ni wa kiafya bora, tambua kwamba unafanya kazi kubwa ya kumpatia mtoto wako mwanzo bora katika maisha. Lakini kama wewe umechoshwa na una lindi la mawazo kuhusu ukubwa wa umbo lako kumbuka kuwa ujauzito ni jambo jema na unafanya vyema mpaka sasa kulea kiumbe ndani yako. Kuwa mwenye faraja kwani zimebaki wiki chache sasa mpaka kujifungua.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 30
Kupata usingizi mzuri usiku kunaweza kuwa kugumu tena zaidi katika miezi mitatu hii ya mwisho. Kadiri tumbo lako linavyokua, kukaa na kujisogeza vizuri inakuwia vigumu.

Unaweza kupata hali ya kubanwa na mkojo mara kwa mara. Hii ina maana nyakati za usiku safari za kwenda chooni zitakuwa nyingi kuliko kawaida. Ndotopia zinaweza pia kuathiri ubora wa usingizi wako, na kukuacha wewe kuhisi kusumbuliwa na uchovu na kushindwa kupumzika. Mnaweza mkazungumza na mwenzi wako kuhusu ndoto zake pia ili kupata wasaa wa kupunguza msongo wa mawazo.