Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 33

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 33
Mpaka sasa, mtoto wako pengine kichwa chake kinaangalia chini katika mji wake wa mimba. Watoto wengi vichwa huangalia chini katika hatua hii, ingawa baadhi wanaendelea kubadili uelekeo.

Mifupa ya fuvu la mtoto wako bado ni laini na haijajiunga kabisa. Hii inafanya kuwa rahisi kwa wewe kumzaa, kwani mifupa katika fuvu la kichwa chake inaweza kuingiliana kidogo yeye akiwa anashuka chini ya uke wako.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 33
Unaweza gundua kwamba miguu yako, mikono, uso, na kifundo cha mguu imevimba kidogo. Uhifadhi huu wa maji unajulikana kama “oedema”. Mara nyingi ni mbaya katika hali ya hewa ya joto na wakati wa jioni.

Cha kushangaza, kunywa maji zaidi, na sio pungufu, ndio itasaidia. Hivyo, kunywa maji! Lakini kamakuvimba kumezidi, na una maumivu ya kichwa, mtafute mkunga au daktari wako mara moja, kwa sababu hizi wakati mwingine ni dalili za “pre-eclampsia”.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 33
Kuhakikisha wewe na mpenzi wako mnakuwa na namba zote muhimu kwenye simu zenu – mkunga, daktari na wodi ya wazazi. Kama una watoto wakubwa, panga na mtu kwa ajili ya kuwatunza kwa siku zile utakazokuwa umeenda kujifungua kwani utashindwa kukihudumia kichanga na kukidhi mahitaji ya watoto wengine wakubwa kwa ufanisi.