Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 37

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya 37
Mtoto wako ameanza kulitoa lile koti la nta nta lilikuwa limeifunika ngozi yake, ingawa bado anaweza akawa na alama za nta nta hii baadhi ya sehemu za mwili wake baada ya kuzaliwa.

Mtoto wako humeza chochote anachokitoa kwenye ngozi yake na hukaa katika utumbo wake mpaka anapozaliwa. Kinyesi chake cha kwanza kitakuwa na rangi ya mchanganyiko nyeusi na kijani, iitwayo “meconium”.

Dalili za ujauzito katika wiki ya 37
Wiki chache zijazo ni mchezo wa kusubiri. Hata hivyo ni vigumu sana kuwa na subira, jaribu kufurahia wakati huu kabla ya mtoto wako hajawasili. Kula vizuri na kupata mapumziko ya kutosha.

ama umechoshwa kuwa na ujauzito, unaweza kuangalia mbeleni na kuwaza kichanga wako atakua na mwonekano gani.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya 37
Je umeshaandaa mfuko wako wenye vifaa vyote muhimu kuwa navyo utakapokuwa unaenda kujifungua? Kama kuna vitu vichache ambavyo hujaviandaa katika dakika za mwisho, usiwe na mawazo, angalia katika orodha yetu ya vitu muhimu kuwa navyo unavyoelekea kujifunua kwenye kituo cha afya.

Andaa nguoambazo mtoto wako atavaa baada ya kuzaliwa na kwaajili ya safari ya kurudi nyumbani. Na kumbuka piakuandaa nguo nyepesi kwa ajili yako mwenyewe.

Hii pia ni nafasi ya mwisho kwa mwenzi au mpenzi wako kurudia kujifunza juu ya jinsi ya kukusaidia unapojifungua na baada ya kujifungua.

Unaweza kumtegemea mpenzi wako kukuongoza wewe katika maamuzi wakati upokwenye uchungu mkali na hautakuwa kwenye hali nzuri ya kutoa maamuzi. Hivyo kumsaidia kumwelewesha ni nini muhimu zaidi mapema ni muhimu.