Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 6

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya sita
Mtoto wako amefikia ukubwa kama wa punje ya choroko. Wiki hii, moyo wake umeanza kupiga. Pamoja na kwamba ni mdogo sana, viungo vyake vimeshaanza kujiunga. Mtoto wako ana kichwa kikubwa na vidoti vyeusi ambavyo macho na pua yake vinakua. Masikio yake yanayochomoza yameshajionesha na mikono na miguu yake inaonekana kama vichipukio vidogo.
Mikono ya mtoto wako ina umbile kama la pedali, na vidole vyake vinajitengeneza hata sasa hivi. Kuna mambo mengi yanayoendelea ndani ya kiumbo chake kidogo pia. Moyo wake umegawanyika katika vyumba vya kushoto na kulia na unapiga mara 150 kwa dakika. Hii ni sawa na mara mbili ya mapigo ya moyo wako.

Dalili za ujauzito kwenye wiki ya sita
Watu wengine kuacha wewe hawawezi kuona ukuaji wa kushangaza unaoendelea ndani ya mwili wako. Lakini wewe utausikia, kwani mabadiliko ya mwili wako yanakuacha ukiwa mchovu na mwenye kichefuchefu.
Kutokuwepo na uwiano kati ya unachokijua na unavyojisikia ukizingatia pia na ambavyo watu wengine kutokujua kinachoendelea mwilini mwako, itapelekea kupata wakati mgumu sana. Unaweza ukawa unajisikia hali ya chini kuliko mwenye furaha. Inakuwa vigumu zaidi kama utakuwa bado hujamshirikisha mtu yoyote kazini kuhusu ujauzito wako, au hata marafiki na familia.

Kufidia hali hii, jitahidi kupumzika vya kutosha ufikapo nyumbani na mshirikishe mwenza wako kuhusu hali yako mara kwa mara. Weka zaidi kipaumbele kwenye kupumzika, na muone daktari kama kichefuchefu kinafanya maisha yako yanakuwa magumu na huwezi kula kitu chochote bila kutapika.
Kufikiria kuhusu jambo lingine wakati huu pia husaidia. Unaweza ukaanza kufikiria kuhusu huduma za ujauzito na aina ya kujifungua ambayo ungependelea. Ni haki yako kuchagua aina gani ya kujifungua unataka.

Unachotakiwa kufahamu katika ujauzito wiki ya sita
Unaweza ukawa unawaza kwamba usumbufu wakati wa usiku utaanza pale tu utakapojifungua. Kusema kweli, usingizi wako unaweza ukaanza kuwa wa utata tangu mwanzo kabisa ya ujauzito. Wakati mwingine sababu ni za kimwili – mfano safari mbili za kwenda kukojoa kila usiku.

Inawezekana matiti kuuma yanakufanya usijisikie vizuri au inaweza ikawa unaamka ukihitaji kula kitu kutokana na njaa. Ni vyema kujitahidi kupangilia mlo wako na kuweza kupata muda mzuri wa kupumzika.
Kama una hamu sana ya kula mara kwa mara jitahidi kujiridhisha bila ya kula sana au kula vyakula visivyo vya afya bora. Unaweza ukachagua vyakula vidogo vidogo (snacks), kama figili, karoti, machungwa au maembe.