Mtandao #1 kwa Afya ya Mama na Mtoto

Address:

P. O. Box 38995, Dar es Salaam, Tanzania

Ujauzito Wiki ya 9

Jinsi mtoto wako anavyokua katika ujauzito wiki ya tisa
Mtoto wako anauzito chini ya gamu 10 lakini yupo katika nafasi kwa ajili ya ukuaji wa haraka. Viungo vya mwili vipo vyote sasa, ikiwa ni pamoja na mikono, miguu, macho, sehemu za siri na viungo vingine, ingawa bado havijakamilika kikamilifu. Placenta (kirutusbisha mimba) inafanya kazi kikamilifu, kwa kuleta virutubisho kwa mtoto wako na kuondoa bidhaa taka zake kuzipeleka kwa mama.

Dalili za ujauzito katika wiki ya tisa
Inawezekana usionekane mjawazito bado, labda kama mimba hii sio ya kwanza kwako. Lakini unaweza kujisikia kuchoka sana na kuumwa, si lazima iwe asubuhi, hivyo ni vyema kujitunza mwenyewe.
Homoni za za ujauzito zinaweza kukuchanganya akili na mwili wako katika kila aina ya njia. Maumivu ya kichwa na mgongo ni mambo mawili ya kawaida ya wewe kutarajia. Kuna baadhi ya dawa kama Ibuprofen na Aspirin ambazo hairuhusiwi kuzitumia kipindi cha ujauzito.

Kufurika kwa homoni mwilini wako kunaweza pia kusaidia kujenga mazingira rafiki kushambuliwa na muwasho na kutokwa na majimaji meupe ukeni (viginal thrush).

Unachotakiwa kufahamu kwenye ujauzito wiki ya tisa
Kuwa mchangamfu kunaweza kukusaidia kuwa na mimba yenye afya njema na kuongeza kasi ya kupata ahueni baada ya kujifungua. Ni vyema kuchagua mpango salama wa mazoezi kipindi cha ujauzito. Ila mazoezi haya yawe si ya kuzidisha.
Ukizungumzia kuwa mchangamfu, ni kawaida kabisa kuwa na wasiwasi kuhusu kama ni salama kufanya ngono katika hatua za mwanzo za ujauzito. Jaribu kutokuwa na wasiwasi. Kwa idadi kubwa ya wanawake ni salama kabisa kufurahia maisha ya ngono yenye kuridhisha katika kipindi cha mimba yako.

Ingawa unaweza kujisikia zaidi kama kutokujisikia kufanya ngono kuliko mpenzi wako kwa wakati huu, wanawake wengi wajawazito huanza kujisikia zaidi kufanya ngono mara baada ya miezi mitatu ya kwanza kupita. Kama ashiki (libido) au matamanio yako yapo chini sana , kuna njia nyingine wewe na mpenzi wako mnaweza kuonyesha upendo wenu kwa kila mmoja bila kufanya ngono.